Naibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Salumu ametangaza kuwa Baraza la
Mitihani la Tanzania, NECTA limesitisha mpango wa kuwafanyia mtihani wa
udahili wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
mwaka huu katika shule za sekondari za serikali.
Usitishaji huo umetokana na wakuu wa shule za serikali kushindwa kukidhi
baadhi ya masharti yaliyotolewa na NECTA, mazingira yaliyopelekea NECTA
kusitisha zoezi la udahili wa wanafunzi hao wanatakiwa kujiung na
masomo kidato cha kwanza.
Ambapo NACTE iliwataka wakuu wa shule kuhakikisha mtihani huo unafanyika
kwa wanafunzi wote wa shule za serikali siku moja na muda uliopingwa,
pia masharti yaliwalazimu wakuu wa shule za serikali kuwasilisha orodha
ya majina ya wanafunzi kwa maofisa elimu wa mikoa na wilaya ili yatumwe
NECTA.
Mazungumzo hayo yalifanyika juzi kwenye kikao cha wadau wa sekta ya
elimu Mkoa wa Morogoro alipokuwa akihitimisha mada yake kwa wajumbe wa
kikao hicho kilichoongozwa na mkuu wa mkoa huo, Dk Stephen Kebwe.
“Necta imewasiliana na wahusika kwa barua rasmi ya kusitisha mtihani huo
ambao ulipangwa ufanyike Februari 28, mwaka huu na wanafunzi wote
waliopangiwa kidato cha kwanza shule mbalimbali za serikali zikiwemo za
bweni, waendelee na masomo kama yalivyopangwa,” alieleza Naibu Katibu
Mtendaji wa Necta.
Post a Comment
karibu kwa maoni