0
Baada ya sauti zilizosambaa zikimuhusisha Mwigizaji Steve Nyerere na Mama wa mwigizaji Wema Sepetu wakizungumza huku akitaja baadhi ya viongozi mbalimbali aliodili nao kwenye sakata la Wema kushikwa na Polisi, leo Steve Nyerere ameita Waandishi wa habari na kuongea nao.

Steve Nyerere amesema kuwa hakuna msanii hata mmoja ambaye anakidai Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema mambo ambayo anasema Weme Sepetu kuwa anakidai chama hicho ni uongo na uzushi mtupu.

Amesema katika wasanii mbalimbali ambao huenda walilipwa pesa nyingi zaidi ni Wema Sepetu pamoja na yeye na kusema wao pamoja na wasanii waliokuwa wanaendesha kampeni ya 'Mama ongea na mwanao' ni wasanii ambao walilipwa vizuri sana na Chama Cha Mapinduzi kuliko wasanii wengine wowote wale.

Steve Nyerere anasema katika mkataba walioingia na Chama Cha Mapinduzi hakuna sehemu mkataba huo unasema ukikamatwa na madawa ya kulevya, bangi  chama hicho kitakuja kukusaidia. 
Pia Steve Nyerere anakiri wazi kuwa sauti ambayo inazunguka kwenye mitandao ya kijamii ni kweli ni sauti yake na alikuwa akiongea vile ili kumridhisha mama yake na Wema Sepetu kwani wakati huo jambo hilo lilikuwa ngumu kwake.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top