0
Mkutano wa Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA na wakazi wa kijiji cha ENDAGAW wilaya ya HANANG mkoani MANYARA umegeuka sherehe baada ya kuzuka mvua kubwa iliyoambatana na upepo.

Mvua hiyo iliyoanza ghafla na kusababisha viongozi kusimamisha hotuba kwa muda ili kujikinga na mvua imeugeuza mkutano huo kuwa sherehe ya kupata mvua.

Mvua hiyo inayoelezwa kuambatana na upepo ilianza wakati Mkuu wa mkoa akimkaribisha Waziri Mkuu kupanda jukwaani ili kuzungumza na Wananchi  na Watumishi wa wilaya ya HANANG.

Baada ya nusu saa mvua hiyo ilipungua na Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA akapanda jukwaani na kuzungumza na Watumishi na Wananchi kwa kuwataka Wananchi kudai mikutano ya mapato na matumizi katika vijiji vyao ili kujua miradi inayotekelezwa katika vijiji vyao.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top