0
Kwa kuthamini vijana na kuwaepusha kuingia katika mambo yasiyostahili katika jamii ikiwemo kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya, mkuu wa mkoa wa Manyara Dk. Joel Bendera maarufu kocha ameanzisha ligi katika mkoa wake iliyopewa jina BENDERA CUP 2017.

Ligi hii inashirikisha timu 16 za mpira wa miguu kutoka mkoani hapa.

Aidha mkuu wa mkoa amekipongeza chama cha soka wilaya ya Babati [BDFA] kwa kuandaa haraka timu shiriki na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada zao za kuendeleza soka hapa mkoani.

Kwa upande mwingine ameskitishwa na ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Manyara kuhamishiwa Arusha kutokana na Vurugu akisema kitendo hicho sio cha kiungwana.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top