Wakazi wa kijiji cha Matufa kata ya Magugu
wilayani Babati mkoani Manyara wameliomba jeshi la polisi kuwashughulikia
watuhumiwa waliokamatwa kwa kumbaka msichana mmoja mwenye miaka 23.
Msichana huyo alibakwa na kundi la wanaume tarehe
3/4/2017 wakati akitokea dukani majira ya saa 2:00 usiku na kusababishiwa maumivu makali ktika sehemu
zake za siri.
Akizungumza na redio manyara biti huyo amesema
alitokea kijana mmoja akamshika mkono huku akimvuta kwa nguvu na alipomuuliza
kwanini unanishika kwa nguvu alimtukana na kuendelea kumvuta akimweleza kuwa
asbishane nae atajua tu kinachofuata.
Anasema alivutwa mpaka kwenye miti mingi ya
mijohoro na kuanza kuvuliwa nguo kwa nguvu na watu waliokuwa zaidi ya sita na
kuanza kumbaka huku akizibwa mdomo na kushikwa miguu.
Anaeleza
kuwa alijaribu kupiga kelele ambapo
msamaria mwema aliekuwa akipita alifika kumwokoa na kufanikiwa kukimbia hali ya
kuwa tayari ameshabakwa na kupata maumivu makali sehemu zake za
siri...clip Binti
Mwenyekiti wa kitongoji cha Kichangani Doglas
Chasusa ni miongoni mwa watu waliofanya
doria usiku kuwatafuta waliofanya uhuni huo anazungumzia tukio hilo.....Clip
Mwenyekiti
Kwa upande wa Baba wa msichana aliebakwa anasema
binti yake alienda dukani ila cha kushangaza alichelewa kurudi nyumbani lakini
hakupata wasi wasi kwa kuwa ni mkubwa na alishapazoea lakini alishangazwa
kumkuta binti yake mlangoni akiwa amezimia hali iliyompa mshtuko ndipo
waliponmpepea na baadae alipozinduka akaelezea kilimchompata huku akishindwa
hata kukaa kwa maumovu makali aliyokuwa akihisi....Clip Baba
Akielezea namna alivyomwokoa binti huyo Shabani
Bello anasema ilikuwa ni vigumu sana kwake kumwokoa lakini alitumia ujasiri
wake kuwatisha lakini walimvamia na kujeruhi kichwani kwa rungu ndipo akapata
nafasi ya kumbana mmoja na wengine wakakimbia.Clip...Shabani
Binti alipata majeraha mabaya sana na hata
kutenguka mkono hali iliyomlazimu kwenda hospitali kufanyiwa vipimo.
Daktari aliekuwepo zamu usiku huo katika kitu cha afya Magugu Abbas Abdala ,
baada ya kumpima alithibitisha kwamba binti huyo kubakwa .
Hata hivyo Polisi waliwakamata watuhumiwa hao
sita waliodaiwa kumbaka msichana huyo, na mpaka sasa wanashikiliwa kwenye kituo
cha Polisi Magugu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Francis Jacob
Masawe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Wanakijiji wa Matufa wameiambia redio manyara fm
kuwa Tukio kama hili liliwahi kutokea tena katika kijiji hicho ambapo mama mmoja
wa alibakwa na kundi la watu wasiofahamika
hadi kufariki.
MSIKILIZE HAPO AKIHOJIWA NA JOHN WALTER.
Post a Comment
karibu kwa maoni