Rais wa Marekani Donald Trump ameaonya kwa mara nyengine kwamba mzozo mkubwa utaibuka na Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa kinyuklia na ule wa kutengeza makombora.
Katika mahojiano na chombo cha habari cha Reuters amesema kuwa angependelea mzozo huo kukabiliwa kidiplomasia lakini amesema hiyo itakuwa vigumu kuafikia.
Bwana Trump alimpongeza mwenzake wa China Xi Jinping akisema amekuwa akijaribu kwa kila njia kuishinikiza Korea Kaskazini.
Awali waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson alisema China imeionya Pyongyang kutarajia vikwazo iwapo itafanya majaribio mengine ya kinyuklia.
Wakati huohuo Korea Kaskazini imetoa kanda ya video ya propaganda ikionyesha itakavyoishambulia Marekani.
Kanda hiyo inashirikisha ikulu ya Whitehouse na ndege ya kubeba ndege za kijeshi inayokabiliwa na inakamilika na ikulu hiyo ikilipuka.
Post a Comment
karibu kwa maoni