0


Msamaha una nafasi kubwa sana katika mapenzi. Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno  hili linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. Hivyo ni vizuri ukawa makini katika matumizi ya neno hili

Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha moyo wako ina maana sana zaidi ya chochote. Samahani itumike tu pale unapotenda kosa moja kwa mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi. Heshima, pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika nakuonekana unajali.

Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja kwa kosa moja ndo mana wanasema,  kosa sio kosa ila ukirudia kosa ndio kosa. Kama ulikua haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako katika matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na ulinganishe na hatua ulizozifanya.

Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku unasema lakinii…… ila……. Siamini kama haya yangetoa……… aina hizi za midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest forgiviness .Utapelekea upande wa pili uliokosewa kukuamini tena na ni rahisi kusamehe na kusahau  tofauti na kuwa na maneno meeengi yakujitetea ilihali umetenda kosa.
Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa upesi

  • Kubali kosa pale ambapo umetenda,NOTE; Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza ,au hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa
  • Badili mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa
  • Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe)
  • Usilazimishe kusamehewa ,yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine.Hapa itategemea na jinsi mlivyo
  • Anayeomba msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila wanakukumbuka, endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa  bahati mbaya.Mfano akikosewa huwa ni mtu wakusema; hiyo ni kawaida yako ina maana anashikilia vitu moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye atakukosea.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top