0
Siku chache baada ya Haji Manara kufungiwa na Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kutojihusisha na shughuli za mpira kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) sama mwaka moja pamoja na faini ya shilingi milioni tisa, msemaji huyo wa Simba
ameandika ujumbe mrefu kwenye mtandao wake wa Instagram.
“Salaam… Namshukuru Mungu kwa sasa masuala yangu binafsi ya kifamilia nimeyamaliza. Naweza sema kitu, kwanza niwape pole nyie kwa haya yaliyonitokea, mimi si mtu ninayeamini uonevu, si mtu ninayeweza kunyamaza nikiona haki inaporwa, si mtu mwenye moyo dhaifu wa kuogopa kukosoa pale panapopaswa kurekebishwa, na always nitabaki hivyo.
Juzi Ijumaa jioni niliambiwa na ofisi yangu imekuja barua toka TFF, ikiniarifu kuna wito wa kunitaka nifike Karume kusikiliza mashtaka dhidi yangu Jumapili asubuhi, wakati huo nikiwa Zanzibar kwa masuala yangu ya kifamilia, na ofisi ikaiandikia TFF barua ya kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hili hadi Jumanne kwa kuwa ntakuwa nipo Dar.
Barua iliwafikia na binafsi nikaongea na Alfred Lucas msemaji wao na akanijibu ameipokea yeye na imegongwa muhuri na katibu mkuu wa TFF keshaipata, kumbuka hiyo ni jioni ya Ijumaaa, Jumamosi nikampigia Alfred kuulizia kikao hicho cha kamati kimepangwa lini, akanijibu Jumatatu ya leo (jana) atanijibu, Jumapili tena mkasikia mliyosikia, ni uharaka upi ilionao TFF wa kushindwa kunipa haki ya kusikilizwa? Natural justice nchi hii haitambuliki!! Wahaini na wauaji nao pia husikilizwa, iweje kwa mtuhumiwa ambae anapigia kelele haki ya mwajiri wake?
Kuna hoja dhaifu inajengwa kuwa nilipaswa nijibu binafsi barua ya TFF , hivi ningewezaje kuijibu barua wakati sikuwepo Dar na sikuwa nimeiona na vipi klabu yangu isiwe na haki ya kunijibia barua, wakati leo imepokwa haki ya kutokuwa na msemaji? na hivi TFF hawajui kuwa mimi nilikuwa naongea kwa niaba ya ofisi na klabu yangu? Nikija sababu za kunifungia nimejiuliza ni kaka yangu huyu msemwa aliyekuwa anasoma hii hukumu?
Nimemuona kwa Millard Ayo, anasoma hukumu ilio kinyume na hati ya mashtaka, hati yao ina makosa mengine na hukumu pia nyingine, ni aina ya hukumu katili zaidi kwa viwango vya mpira wetu, ila nawaambia TFF Haji hajawahi kuwa dhaifu wa moyo, anaweza kuwa dhaifu wa kiwiliwili, lakini nina moyo wa Simba, ntapambana kwa kiwango cha juu sana, ntadai haki yangu na ya mwajiri wangu kwa viwango, na ntaziomba kamati zao zipokee rufaa yangu na kukaa kwa uharaka huu walionifanyia, na nipewe haki ya kusikilizwa, nisihukumiwe kishabiki wala kwa chuki, na nawahakikishia kikao kitakachokaa.
“Hivi ndivyo alivyoandika Haji Manara kwenye Instagram yake.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top