Mzee Selemani Mwaipopo alieathirika kwa kuchomwa sindano yenye virusi vya Ukimwi akiwa mfungwa huko Congo DRC.Picha na John Walter |
Akiwa katika gereza huko Congo hakuweza kuwasiliana na mtu yeyote kutoka Tanzania hadi pale wanajeshi wa hapa nchini walipofika huko mwaka jana katika kutuliza ghasia nchini humo na kutaka kujua kama kuna watanzania wanaoshikiliwa katika Gereza nchini Humo ndipo akagundulika Selemani Mwaipopo.
Mzee Selemani Mwaipopo alieathirika kwa kuchomwa sindano yenye virusi vya Ukimwi akiwa mfungwa huko Congo DRC.Picha na John Walter |
Akizungumza na Manyara Fm katika kipindi cha Tuzungumze kinachoendeshwa na John Walter Mwaipopo amesema anachokumbuka aliacha mke mmoja na mtoto mmoja amabo wote kwa sasa wameshapoteza maisha.
Alipoulizwa kama anao ndugu zake anao wakumbuka amesema kuwa aliwaacha ndugu zake Babati enzi hizo ikiitwa Mbulu mkoa wa Arusha kabla ya kupanda hadhi na kuwa mkoa wa Manyara lakini kwa sasa amepata taarifa kuwa wapo Simanjiro.
Selemani mwaipopo kwa sasa anatumia Vidonge vya ARV na pia anao ugonjwa wa TB hivyo anaomba yeyote anaeguswa na matatizo yanayomkabili amsaidie kwa hali na mali kwani hana hata pa kuishi.
Mzee Selemani Mwaipopo alieathirika kwa kuchomwa sindano yenye virusi vya Ukimwi akiwa mfungwa huko Congo DRC.Picha na John Walter |
Kwa ulieguswa na jambo hili tafadhali toa mchango wako kupitia namba ya tigo 0657 932 500.
MSAIDIE LEO USAIDIWE KESHO KWANI MATATIZO NI KWA KILA MTU.
Post a Comment
karibu kwa maoni