Emmanuel Warioba (26) ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumfanyia ukatili mwanae kwa kumpiga fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo wilayani Kwimba.
Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mwanza, DCP: Ahmed Msangi inaeleza kuwa Aprili 21 mwaka huu majira ya saa 16:oo katika kijiji cha Mwamakoye, Kata ya Mwakilyambiti Tarafa ya Nayamilam,a wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, inadaiwa kuwa mtu aliyejulikana kwa jina la Emmanuel Warioba (26), mwalimu wa shule ya Mwamakoye anashikiliwa na jeshi hilo kwa kumfanyia ukatili huo mwanae aliyejulikana kwa jina la Sifael Emmanuel(8) mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule hiyo.

Hata hivyo wananchi walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio hilo ambapo Polisi walifanya ufuatiliaji wa haraka katika eneola tukio na kumkamata mtuhumiwa . Ambapo mpaka sasa mtuhumiwa yupo katika mahojiano na jeshi la Polisi na uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Ngudu kwa ajili ya uchunguzi huku pindi uchunguzi utakapo kamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwaajili ya mazishi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi ametoa wito kwa wazazi au walezi kuangalia namna ya kuwaelimisha watoto wao katika kuwapa maadili mema kuliko kutoa adhabu ambazo zingine hupelekea madhara kwao na kusababisha kifo.
Post a Comment
karibu kwa maoni