Wakazi wa Arusha nchini Tanzania wakisheherekea
azimio la kilimanjaro katika maadhimisho ya siku ya ukombozi wa Africa.
Siku ya maadhimisho
ya ukombozi wa Afrika,mwaka huu imesheherekewa kwa kuzinduliwa rasmi
azimio la kilimanjaro ambalo ni mwamko wa waafrika katika kupigania
haki, amani na heshi
Afrika arising au mwamko wa Afrika ni
harakati zinazo waunganisha waafrika kupitia mitandao ya
kijamii,majukwaa,makongamano na matamasha ambayo yameandaliwa na makundi
mbalimbali ya kijamii katika nchi mbalimbali za Afrika.
Baadhi ya vijana,mjini Arusha nchini Tanzania, wakisheherekea siku ya ukombozi wa Afrika
Misingi ya harakati hizi ambazo zinawasilishwa kwa njia ya Amani ni kusisitiza haki za msingi kwa waafrika kutoka kwa viongozi wao na serikali zao .
Pamoja na kuwa harakati za Afrika zilikuwepo wakati wa kupigania uhuru lakini sasa mwamko wa Afrika ,unataka kulaani unyonyaji wa raslimali na mali asili ,ukandamizaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Post a Comment
karibu kwa maoni