
Taarifa ya Singida United imesema mchezaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili usiku wa Jumatatu na Jumanne mchana anatarajiwa kutambulishwa rasmi.
Atupele anajiunga na Singida United baada ya klabu yake, JKT Ruvu kushuka daraja katika msimu ambao alijiunga nayo kutoka Ndanda FC ya Mtwara
Atupele ni mfungaji bora wa Kombe la Shirikasho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) mwaka jana, kabla ya mwaka huu kupokonywa na heshima hiyo na Mzambia, Obrey Chirwa wa Yanga.
Na kumsajili Atupele ni mwendelezo wa Singida United kusajili wachezaji nyota wa nyumbani na nje ya nchi ili kutengeneza kikosi kikali cha ushindani msimu ujao.
Tayari Singida iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaye kocha mzoefu, Mholanzi Hans van der Pluijm iliyemchukua Yanga.
Post a Comment
karibu kwa maoni