Halmashauri ya
mji wa Babati imeshauriwa kuchimba visima vya maji katika eneo la Maisaka
katani inapotarajiwa kujengwa kwa kituo cha mabasi wakati wanasubiri kupata maji kutoka Darakuta
mradi kutoka Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira [BAWASA].
Pia imeelezwa
kuwa kutoa maji eneo la Darakuta [long plan]lililopo zaidi ya Kilometa 20
kutatumia mabilioni ya pesa.
Ushauri huo
umetolewa na katibu mkuu ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa [TAMISEMI]
Eng.Mussa Iyombe alipotembelea eneo hilo la Katani na kushuhudia pakiwa na
msitu huku kukiwa hakuna dalili yeyote ya kuanza ujenzi.
Mkurugenzi
wa mji wa Babati Fortunatus Fwema alieleza mbele ya katibu mkuu kuwa tatizo lililopo katika maeoneo hayo ni
kukosa wanunuzi wa viwanja huku Katibu akieleza kuwa hata kama ni yeye
asingeweza kununua kiwanja maeneo hayo
ya katani ambayo hayana huduma za maji wala umeme.
Amemtaka mkurugenzi na watumishi wengine kutimiza wajibu wao kwa wakati na sio kulalamika.
Ikumbukwe kuwa
kwa sasa Halmashauri ya mji wa Babati haina kituo cha mabasi baada ya kituo
kilichopo kukabidhiwa kwa chama cha Mapinduzi.
Kufuatia hatua
hiyo Halmashauri imepanga kuanza na kituo cha muda kwa kujenga kibanda kwa
ajili ya abiria kufikia na choo huku wakichukua
maji kwa gari hatua ambayo katibu amesema ni kufeli.
Post a Comment
karibu kwa maoni