Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma
Wizara ya Fedha na
Mipango imeliomba Bunge iidhinishie makadirio ya mapato na matumizi (Bajeti) ya
zaidi ya shilingi trilioni 11.757
ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu
yote 9 yaliyochini ya Wizara hiyo.
Maombi hayo yametolewa na Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, wakati akiwasilisha makadirio ya
mapato na matumizi ya Wizaya hiyo, Bungeni Mjini Dodoma, leo.
Dkt. Mpango amesema kuwa kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 10.328 ni kwa ajili
ya matumizi ya kawaida na shilingi
trilioni 1.429 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.
Amefafanua kuwa
Matumizi ya Kawaida yanajumuisha shilingi bilioni 87.996 kwa ajili ya mishahara, shilingi bilioni 778.612 kwa ajili ya matumizi Mengineyo (OC) na shilingi trilioni
9.461 ni kwa ajili ya kulipa Deni la Taifa na Huduma nyingine.
Post a Comment
karibu kwa maoni