0
The moonKukamilika kwa mwezi mtukufu wa Ramadan ni likizo kuu ya kidini ya Eid al-Fitr, ambapo waislamu kote duniani hukusanyika kwa sherehe za kumaliza mwezi mtukufu.
Hata hivyo wakati wa siku kuu hiyo kubwa takatifu ya kiislamu inapowadia, wengi wa waislamu bilioni 1.8 huwa na matumaini kupata ishara ya kushiriki sherehe hizo.
Waislamu hufuata kalenda inayoambatana na mwezi.
Sherehe za Eid zaanza Kenya
Sherehe za Eid zaanza Kenya
 Waislamu hufunga wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan na kujizuia kula chakula na kunywa kuanzia asubuhi hadi jioni.
Ikiwa mwezi huu ungefuata kalenda ya jua, watu ambao wanaishi sehemu fulani za dunia wangesherehekea Ramadan yao msimu ya joto huku wakiwa na siku ndefu ya jua, huku sehemu zingine za dunia zikiwa na vipindi vifupi vya misimu ya baridi.
Lakini ndani ya dini ya kiislamu kuna mdahalo kuhusu ni lini sherehe hizo zinastahili kuanza.
Waislamu kwenye nchi nyingi hutegemea habari kuhusu kuonekana kwa mwezi mpya badala ya kuangalia angani wao wenyewe.
Wengine hufuatilia kalenda ya mwezi, huku wengie nao wakifuatilia sayansi ya angani kutangaza kuonekana kwa mwezi mpya.
Kwa hivyo tarehe za Eid hutofautiana kote duniani, licha ya kuwepo tofauti ya siku moja au mbili hivi.
Kwa mfano mamlaka nchini Saudi Arabia, yenye waislamu wengi wa Sunni, hutangaza kumalizika mwezi wa Ramadan, kutokana na maoni ya watu ambao huona mwezi mpya.
Kisha waislamu kwenye nchi zingine hufuata mkondo huo.
Lakini nchini Iran yenye waislamu wengi wa Shia hutegemea matangazo ya serikali.



Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top