0
Watu 123 wameteketea hadi kufa nchini PakistanTakriban watu 140 wamethibitishwa kufa, baada ya lori lililokuwa likibeba mafuta na lililopata ajali ya barabarani kushika moto na kuteketea nchini Pakistan.
Watu wengine kadhaa wameteketea vibaya, pale walipokuwa wakijaribu kuteka mafuta kutoka katika lori hilo la mafuta.
Waliojeruhiwa wanatibiwa hospitali. Wazima moto wamo katika eneo la ajali wakijaribu kukabiliana na moto huo.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa zasema kuwa, lori hilo la mafuta lililokuwa likiendeshwa kwa kasi, lilipinduka, kuanguka na kisha kushika moto.Ramani ya Pakistan
Mashuhuda wanasema kuwa, baadhi ya watu waliofika katika eneo la ajali walikuwa wakivuta sigara, jambo ambalo linakisiwa kuwa chanzo cha moto huo, hiyo ni kwa mjibu wa runinga ya Geo TV ya Pakistan.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top