0


TANZANIA
imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya COSAFA Castle
baada ya ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Lesotho kufuatia sare ya 0-0
ndani ya dakika 90 usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg,
Afrika Kusini.


Shujaa
wa Taifa Stars leo amekuwa golikipa Said Mohammed Mduda aliyepangua
penalti ya Nahodha wa Mamba, Thapelo Mokhehle baada ya Sera Motebang
kugongesha mwamba wa kulia mkwaju wake na kurudi uwanjani.


Waliofunga
penalti za Lesotho ni Hlompho Kalake na Tsoanelo Koetle wakati Shiza
Kichuya aligongesha mwamba wa juu penalti ya kwanza ya Tanzania, kabla
ya Nahodha Himid Mao,Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Daudi kumtungua
kipa wa Mamba Samuel Ketsekile kuipatia Taifa Stars ushindi mzuri wa
4-2.


Ushindi
unakuja siku 25 baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 Juni 10, mwaka
huu katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi L kufuzu Kombe la Mataifa ya
Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.


Katika
mchezo huo uliochezeshwa na refa Romeo Kasengele wa Zambia,
aliyesaidiwa na washika vibendera Thomas Kusosa wa Zimbabwe na Helder de
Carvalho wa Angola, ndani ya dakika 90 timu hizo zilishambuliana kwa
zamu, Lesotho wakitawala zaidi kipindi cha kwanza na cha pili Taifa
Stars wakazinduka.


Kutoka
na ushindi huo, Tanzania inaondoka na dola za Kimarekani 10,000 zaidi
ya Sh. Milioni 22 kwa fedha za nyumbani, wakati Lesotho wamepata dola
8,300.


Fainali
ya COSAFA Castle 2017 itachezwa Jumapili Uwanja wa Royal Bafokeng,
Phokeng mjini Rusternburg baina ya majirani, Zambia na Zimbabwe na
bingwa atapata dola 42,000 na mshindi wa pili dola 21,000.


Kikosi
cha Tanzania kilikuwa; Said Mohammed, Shomary Kapombe, Gardiel Michael,
Nurdin Chona, Salim Mbonde/Abdi Banda dk61, Salmin Hoza/Muzamil Yassin
dk61, Himid Mao, Simon Msuva, Raphael Daudi, Stahmili Mbonde/Elias
Maguri dk71 na Shiza Kichuya.


Lesotho;
Samuel Ketsekile, Itumeleng Falene, Motlomelo Mkwanazi, Thapelo
Mokhehle, Bokang Sello, Kefuce Mahula/ Hlompho Kalake dk89, Tumelo
Khutlang, Tsoanelo Koetle, Napo Matsoso, Jane Ntso/ Mabuti Potloane dk59
na Sera Motebang.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top