0


Image result for kamanda masawe 
Jeshi la polisi mkoa wa Manyara limekataza maandamano ya BLACK THURSDAY yaliyopangwa kufanyika nchi nzima hii leo.
Akizungumza na WALTER HABARI asubuhi leo Agust 31 Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Francis Masawe amesema kuwa hawajapata taarifa yeyote kuhusu maandamano hayo hivyo hayatafanyika.
‘Hakutakuwa na maandamano yeyote na endapo watafanya watakuwa wanatuchokoza’alisema Kamanda Masawe.
Mwenyekiti wa Baraza la vijana wa Chadema mkoa wa Manyara Frank Oleleshwa amesisitiza kuwa watafanya maandamano hayo huku akiwataka vijana na wananchi wengine wajitokeze kuwaunga mkono.
‘Mkoa wa Manyara unaunga mkono kauli ya mwenyekiti wetu wa Taifa kwamba siku ya leo tunaitangaza kama Lhamisi nyeusi kupinga polisi kukamata viongozi wetu ovyo’.
Aliongeza kuwa wameshaliandikia jeshi la polisi barua na mpaka sasa bado hawajajibiwa ila halitawazuia wao kufanya maandamano yao ya amani.
Wiki iliyopita, baraza hilo la vijana lilitangaza kuwepo kwa maandamano ya amani siku ya kesho ambayo waliyapa jina la “Black Thursday” yenye lengo la kushinikiza kuwepo kwa haki za kisiasa, kiuchumi, utawala wa sheria pamoja na haki za binadamu nchini.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top