Basi la kampuni ya Sharon lenye namba
za usajili T 349 lililokuwa litatoka Dodoma kwenda Arusha, limepinduka eneo la
mabanzini-Bohay mjini Babati na kusababisha vifo vya watu wawili huku wengine
wakijeruhiwa.
Majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa
hospitali ya Mrara mjini Babati kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara
Francis Masawe akizungumza juu ya ajali hiyo amesema kondakta na mtoto mdogo
ndiyo walifariki huku 11 wakijeruhiwa.
Hata hivyo waliofariki bado
hawajafamika kwa majina.
Chanzo cha ajali hiyo ni kona kali
zilizopo kwenye bara bara bara hiyo inayofanyiwa matengenezo.
Shuhuda wa karibu katika ajali hiyo aliyejitambulisha
kama Toto Wa Bonga anasema ‘Nilifika
kama dakika kumi baada ya ajali ni uzembe usio na na kiwango baada ya kupata
Chai Mjini Babati dereva alimpa gari konda aliendeshe baada ya kumaliza msitu
wa Haraa kona ya kwanza kali ukitokea Boay ikamshinda gari ilikuwa mbio sana
wakati wa kukata kona matairi ya upande moja yaliinuka na kupoteza mwelekeo na
kuanguka konda mwenyewe amekufa dereva amekimbia mimi nilikuwepo hadi police
kutoka kituo kidogo cha Bonga alipofika akibebwa na pikipiki hayo ndiyo mapokeo
kutoka kwa wasafiri ni bora uchunguzi uanzie hapo.”alisema shuhuda huyo.
Aidha kamanda amesema
atazungumza na mamlaka zinazohusika na kutoa vibali ili waizuie bara bara hiyo
kutumika kwani bado kwa sasa haipo vizuri kwa magari kupita haswa ya abiria.
Katika hatua nyingine ameuambia
mtandao huu kuwa ajali ndani ya mkoa wa Manyara zimepungua kwa kiwango kikubwa
bila kutaja ni kwa asilimia ngapi.
Post a Comment
karibu kwa maoni