0


Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk Adelhelm MeruSerikali  imesema kwamba viwanda inavyovichukua ni vile vilivyoshindwa kutimiza wajibu wa uzalishaji na kuongeza ajira nchini.
Akijibu tuhuma zilizotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jumatatu iliyopita kuwa serikali inafanya makosa kuchukua viwanda vilivyobinafsishwa na kushindwa kuanzisha viwanda vipya nchini, Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk Adelhelm Meru (pichani) amesema madai ya Chadema siyo ya kweli na alitoa mifano ya viwanda vilivyoanzishwa katika awamu ya tano.
“Kwa sababu hiyo zoezi la kuvirejesha vile vilivyovunja mikataba halina ubaya wowote kama ilivyodaiwa na Chadema,” aiongeza. Akijibu hoja ya Chadema kwamba hakuna viwanda vipya katika Serikali ya Awamu ya Tano, Dk Meru alishangazwa na hoja hiyo na kusema kuna viwanda vilivyojengwa na vinavyoendelea kujengwa kwa mikopo ya taasisi za kifedha za ndani.
Alitaja mifano ya viwanda hivyo kuwa ni Pipeline Industries, Global Packaging, Masasi Food Industries, CATA Mining Ltd. Kadhalika alisema katika kipindi hiki, jumla ya viwanda vilivyosajiliwa na kuanza utekelezaji kupitia TIC ni 224, kupitia EPZA ni 41 na kupitia BRELA ni 128 na kuongeza kuwa jumla ya viwanda vidogo na vya kati vilivyoanzisha na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) ni 2,243.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top