0
Klabu ya soka ya Majimaji ya mkoani Ruvuma imejinasibu kuwafunga mabingwa watetezi wa VPL Yanga kwenye mchezo wao wa kesho.
Majimaji kupitia kwa mjumbe wake wa kamati ya utendaji Salum Masamaki wamesema wamejiandaa vyema chini ya mwalimu Habib Kondo na wanaamini watapata ushindi katika mchezo wao wa kwanza kwenye uwanja wao wa nyumbani.
"Tumejiandaa vyema na mchezo tutaifunga Yanga bila shida kwasababu timu yetu iko vizuri ndiyo mana tumetoa sare moja na kupoteza mchezo mmoja lakini michezo yote tumecheza ugenini", amesema Masamaki.
Katika hatua nyingine Masamaki amethibitisha kuwa kocha wao Kally Ongala hayupo na timu kwasababu mkataba wake unamalizika mwezi Oktoba hivyo bado anaongea na wadhamini ambao ni GSM ili kuona kama ataongeza mkataba.
Majimaji ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo wa VPL ikiwa na alama moja baada ya michezo miwili na itakuwa nyumbani kesho kucheza na Yanga kwenye raundi ya tatu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top