0
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amezindua Kitabu cha Mwongozo kwa
Wanamipango Tanzania, kilichoandaliwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini
kwa kushirikiana na Taasisi ya Mafunzo ya Jamii ya nchini Uholanzi (ISS), na
kuwataka wataalamu wa mipango hapa nchini kuandaa mipango yenye tija
itakayoiwezesha jamii kuondokana na umasikini.

Dkt.
Kijaji ameeleza kuwa nafasi ya wataalamu wa mipango katika kukuza uchumi wa nchi
ni kubwa na kwamba kinachotakiwa ni kuandaa mipango shirikishi itakayochangia
kuimarisha maisha ya wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi.

“Ni
matumaini yangu makubwa kwamba kuzinduliwa kwa kitabu hiki cha mwongozo kwa
wanamipango, kutakuwa chachu ya wataalamu wetu kuangalia namna ya kupeleka
maendeleo vijijini na sehemu nyingine duniani kwa kutoa wataalamu waliobobea
ili kuharakisha maendeleo ya nchi” alisistiza Dkt. Kijaji

Ameeleza kuwa maudhui
ya kitabu hicho yapelekwe hadi ngazi za chini kupitia Serikali za Mitaa ili
watu wengi waweze kukisoma na kuelekezwa namna bora ya kupanga mipango yao ya
maendeleo.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top