0






Wakazi Wa Kijiji Cha Nakwa Kilichopo Wilayani Babati Mkoani
Manyara Wamelalamikia  Halmashauri Ya Mji
Wa Babati  Kwa Kuwakabidhi Mradi Wa
Maji  Uliochini Ya Kiwango  Ambao Ulitarajiwa Kuhudumia Wakazi   Elfu Tano [5000]  Wa Kijiji Hicho  Lakini 
Mradi Huo Kwa Sasa Ni Kilio  Kwa
Wananchi  Kutokana Na Maji Kutopatikana
Kama Walivyo Tarajia .
Mradi Huo Unaolalamikiwa Kwa Kuwa Chini Ya Kiwango  Unadaiwa Kutumia Millioni 800.1  Huku Miundo Mbinu Yake Ikiwa Haiwezi Kuhimili
Kupitisha Maji Kwa Muda Mrefu Hali Inayosababisha Kupasuka  Kwa Mabomba  
Na Wakazi Kuendelea Kuteseka Kwa Kukosa Maji Ambayo  Yamekuwa Yakitoka Kwa Zamu  Huku Vituo Vingine Vikielezwa Kutokutoa Maji
Toka Mradi Huo Uanze.
Hatahivyo Muhandisi Wa Mradi Huo Ernest Kakore Amesema Kuwa
Wananchi Bado Hawajaonesha Kuupenda Mradi Ndomana Unapelekea Kuwa Na
Changamoto.
Naye Mkurugenzi Halmashauri Ya Mji Wa Babati Fortunatas
Fwema Amekiri Kuwa Mradi Bado Unalalamikiwa Na Wanakijiji  Kutokana Na Baadhi Ya Taratibu
Kutokutekelezwa   Kwani Aliwahi
Kutembelea Mradi Huo Na Wataalamu Wa Maji 
Na Kuptia Vikao Mbalimbali Wamemwandikia Kamanda Wa Taasisi Ya Kuzuia Na
Kupambana Na Rushwa[ Pccb] Kwa Ajili Ya Uchunguzi Zaidi.
Hivi Sasa Ni Takribani Miezi Sita  Toka Kuzinduliwa Kwa Mradi Huo Na Mkuu Wa Mkoa
Wa Manyara Dr. Joel Bendera  Lakini Bado
Mafanikio Hayajaonekana.


Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top