0






Mbunge mteuliwa wa chama cha wananchi (CUF), Bi Hindu Mwenda
amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa
matibabu.
Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na
Mawasiliano wa CUF, Abdul Kambaya imesema kuwa Bi Hindu amefariki jana jioni
baada ya kuugua kwa siku kadhaa japo hajaeleza kiundani chanzo cha kifo chake
lakini amesema taratibu nyingine zinazofuata zitaelezwa hapo baadaye.
Marehemu Bi Hindu alikuwa ni miongoni mwa wabunge
wapya waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi ya wabunge nane ambao
walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge na Mwenyekiti wa CUF,
Profesa Ibrahim Lipumba

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top