0

Jeshi la polisi mkoa wa Manyara kwa kujali na kutambua umuhimu wa Michezo katika jamii wamekuletea Michuano ya soka itakayozikutanisha timu zisizopungua ishirini ndani ya mkoa.
Ligi itafunguliwa rasmi September 16 2017 ambapo inatarajiwa kuwa na mechi mbili  kila siku katika vituo viwili,cha  Magugu na Babati mjini uwanja wa Kwaraa.
Michuano hii ilikuwa ianze agosti 5 mwaka huu lakini zikatokea dosari hapo kati kati na  kulazimika kusogezwa mbele.
Taarifa za uhakika ilizozipata JOHNWALTER HABARI ni kwamba michuano hiyo itaanza siku ya jumamosi na kufunguliwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Francis Masawe. 
Uslama Cup kw mwaka huu imebeba Ujumbe mkubwa kwa jamii Katika kutii sheria bila shuruti,kupinga ujangili,kupinga mimba mashuleni, pamoja kutunza mazingira na misitu kwa lengo la kuifanya jamii iwe na uelewa wa mambo hayo muhimu.
 Usalama cup 2017 imeandaliwa na kuratibiwa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na  wadau mbalimbali Maendeleo Mkoa wa Manyara.
Wadau hao ni:


EXPORT TRADE
CHEM CHEM COMPANY
TANZANIA POSTAL BANK  TAWI LA BABATI
BAJWA COMPANY
DODOMA TRNPOT
POLE POLE BUS SERVICE
FIRST AND LAST BAR
MAFUNGU AGROVET
CRDB BANK TAWI LA BABATI MJINI
MANUU COMPANY
LALAA GALAPO
MAMA ANGO.

MATOKEO YOTE LIVE ON WALTER HABARI,ARUSHA 24 NEWS NA JOHNWALTER BLOG
KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU NAMBA 0657932500
 

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top