0


Mkurugenzi wa shule za  Rift Valley Babati kushoto Henrislaus-Laus Mallya,kushoto ni Afisa taaluma shule za sekondari mkoa wa Manyara Lago Sillo katika sherehe za mahafali ya darasa la saba na kidato cha nne ya shule ya Rift Valley Babati.

onyo kali limetolewa kwa watumishi wa Imani za dini  wanaofika kutoa neno kwa wanafunzi katika shule mbalimbali hapa nchini na kuwashawishi wanafunzi kuhama katika imani walizonazo na kufuata imani zao.
Onyo hilo limetolewa na Afisa taaluma shule za sekondari  mkoa wa Manyara Lago Sillo  wakati akizungumza na wazazi na wanafunzi kwenye mahafali ya darasa la saba na kidato cha nne katika shule ya Rift Valley Babati.
Sillo amewataka watumishi hao wa kiimani kufanya kile walichokusudia kuwafikishia wanafunzi hao, na sio kushawishi wanafunzi kuachana na imani walizonazo kwani jambo hilo linaweza kuleta taswira nyingine baina ya dini.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Shule ya msingi na Sekondari Rift Valley Babati ndugu Henrisalus-Laus Mallya amewataka Wazazi na walezi wa  watoto waliohitimu darasa la saba na wanaotajia kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka huu wametakaiwa kuwa karibu na watoto wao ili wasijiingize katika vishawishi na makundi mabaya ili kufikia malengo yao.
Aidha amempongeza mkurugenzi wa shule hiyo ambae pia anazo shule nyingine mkoani kilimanajro pamoja na vyuo vya ualimu kwa jitihada alizoonyesha katika kuwekeza kwenye Elimu, akiwataka na wengine kuiga mfano huo.
Akizungumzia ufaulu amesema kama shule imeshindwa  kushindana kimkoa haina haja ya kushindana na wengine wanaofanya vizuri ila ijipange upya.
Naye mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Rift Valley Babati Dadly Wilfredy Mallya akizungumzia suala la uwepo nidhamu mbaya  kwa baadhi ya  wanafunzi  amesema kwa kiasi kikubwa inachangiwa na utandawazi.
Mallya amewaomba wazazi washirikiane na walimu ili kuweza kuwajengea nidhamu bora wanafunzi pindi wanapokuwa nymbani na shuleni pia.
Historia ya shule  ya Msingi na Sekondari Rift Valley Babati ilianzishwa rasmi mwaka 2003 ikiwa na wanafunzi 21 lakini mwaka 2012 ikaingia kwa msimamizi mwingine na katika mwaka huo shule iliendelea kupata wanafunzi na mpaka sasa ina kuna wanafunzi 353.
Kwa mahafali ya jumamosi ya  leo septemba 30 2017, kwa darasa la saba ni mahafali ya tisa na kwa kidato cha nne ni mahafali ya nne.Shule ipo Mtaa wa Muruki,kilomita 2 tu kutoka stand ya mabasi Babati,ni shule ya kutwa na Bweni yenye michepuo ya Sayansi,Biashara na Sanaa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top