0
Image result for mbowe
Viongozi mbalimbali wa kisiasa,dini na serikali walifika katika safari ya mwisho ya Baba yake mzazi Paulina Gekul aliezikwa nyumbani kwake Dareda wilayani Babati mkoani Manyara.
Viongozi wa kisiasa waliohudhuria ibada hiyo ya Mazishi ya Mzee Philip Gekul ni pamoja na mwenyekiti wa Chadema Freema Mbowe ambaye alitokea jijini Nairobi akiendelea kumhudumia kwa karibu Mheshimiwa Tundu Lissu aliepigwa risasi ziadi ya tano katika maeneo mbalimbali ya mwili wake na watu wasiojulikana mjini Dodoma zinapofanyika shughuli za Bunge.
Baada ya kushiriki ibada ya mazishi Mbowe alipata nafasi ya kuzungumza na waandishi wa Habari kuhusu afya ya Lissu kwa sasa na fedha walizoahidi serikali kumtibia.
Freeman Mbowe amesema mpaka sasa hali ya Lissu inaendelea kuimarika na ameshafanyiwa upasuaji zaidi ya Mara 14.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top