0
Kumekuwa na maswali mengi sana kuhusu mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo katika shughuli za Maendeleo ndani ya mkoa wa Arusha anazozifanya ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wananchi wenye shida mbalimbali.

Mbunge wa Arusha mjini kwa msimu wa pili mfululizo kupitia tiketi ya  [CHADEMA] Godbless Lema anasema kazi hizo anazofanya Mkuu wa mkoa ni kwa ajili ya kujiimarisha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ili kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya CCM.

Gambo amelijibu hilo mbele ya waandishi wa habari akiwa ofisini kwake kwamba hana wazo lingine zaidi ya hiki anachokifanya kw sasa kama mkuu wa mkoa kwani hiyo ndio kazi yake.

Rc Gambo ameongeza kuwa yeye ni mkuu wa mkoa na watendaji wote wa serikali wakiwemo wabunge wote wa mkoa wa Arusha bila kujali ni wa chama gani wapo chini yake.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top