0

BUNDA:Zaidi ya ng’ombe700 katika kijiji cha Rwabu katika Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara Wamekufa na wengine kubaki katika hali tete












#GHAROS RIWA -BUNDA.

Zaidi ya ng’ombe700 katika kijiji cha Rwabu katika Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara  Wamekufa na wengine kubaki katika hali tete BUNDAkwa madai ya kukosa maji na nyasi  kwa muda mrefu.
Hayo yamesemwa na wafugaji  wa kijiji hicho wakati wakizungumza na redio mazingira fm katika ofisi ya mtendaji wa kijiji ambapo wameeleza kuwa tatizo hilo limetokana  na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Kisale Mgalula ni mwananchi wa kijiji hicho amesema kuwa kufauatia hali hiyo amepoteza ng’ombe 50 kwa kukosa maji na nyasi jambo analodai kuwa ni hasara kubwa zaidi kwake kuwahi kutokea.
Naye Mzee kafungilo Buzuri ameiambia redio hii kuwa amepoteza ng’ombe 30 kwa kukosa maji na kutembea umbali mrefu kutafuta malisho.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha rwabu bwana Gelad Kuzenza, amesema kwa makisio ya chini walikuwa na ng’ombe 1500 na kwa sasa wamebaki 700 huku akieleza kuwa  bei ya ng’ombe aliyekuwa akinunuliwa kwa shilingi 400,000 hivi sasa ni shilingi 15,000 hadi 30,000 tena kwa kubembeleza wateja.















Aidha ameiomba serikali kuwasaidia kuwachimbia bwawa kusaidia afya ya mifugo na binadamu kwakuwa wakazi wa kijiji hicho ni wakulima na wanategemea mifugo hiyo kama wanyamakazi kufanikisha shughuli za kilimo hivyo kwa sasa hawawezi kutumia tena kwani mifugo hiyo imekonda zaidi na mingine ikilala zizini ni lazima inyanyuliwe ndiyo iweze kuinuka.
Amesema kutokana na mifugo yao kuwa na hali mbaya wanaiomba serikali kuwapelekea trekta za kukodisha kwa bei nafuu ili kufanikisha kilimo kwa msimu huu wa 2017/18.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top