0
GHAROS RIWA & THOMAS MASALU.
Bunda.
Zikiwa zimesalia wiki moja wanafunzi wa kidato cha nne nchini kote kuanza mtihani wao wa taifa wazazi na walezi wametakiwa kuwa na desturi ya kuwalea watoto wao katika maadili mema na kuacha kuwatuma kwenda kununua mahitaji mbalimbali dukani nyakati za usiku kwani kufanya hivyo ni kutoa mwanya kwa watoto hao kukutana na watu wanaoweza kukatisha ndoto zao kwa kuwapatia mimba.
Hayo yamesemwa jana na mgeni rasmi katika mahafari ya 24 katika shule ya sekondari bunda mheshimiwa diwani wa kata ya kabarimu Pastory Ncheye.
Amesema suala la mimba linatokana na wazazi kutowajengea malezi mazuri watoto wao, na kutolea mfano kuwa mzazi anapomtuma mtoto kwenda kufanya biashara usiku au kununua bidhaa usiku dukani inapelekea watoto hao kukutana na watu wanaowashawisha kushiriki nao kufanya ngono hatimae kupata mimba.
Aidha amewatahadharisha wanafunzi kuacha kujihusisha na vitendo vya ngono kwani kupata mimba ni majaliwa lakini watambue kwamba kuna gonjwa hatari la ukimwi.
Mheshimiwa ncheye katika mahafari hayo ameaidi kushirikiana na shule hiyo kurekebisha gari la shule lililoaribika kwa  muda mrefu hivyo kuitaji fedha zaidi ya shilingi milioni moja kukamilika.
Pamoja na hayo pia ncheye ameaidi kuwapelekea miche ya miti ili kuhakikisha mazingira ya shule hiyo yanaendelea kuwa mazuri na ya kupendeza, na kuwasifu kwa jitihada walizozifanya za usafi wa mazingira.
Kwa upande wake mwalim mkuu wa shule hiyo Machota Kora katika risala yake amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya upungufu wa matundu ya vyoo, vyumba vya madarasa, pamoja na uzio katika mabweni ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Hata hivyo amewaomba wazazi na walezi kushirikiana na walimu katika kuwalea watoto kwakuwa wao wenyewe hawawezi na ndiyo maana katika shule hiyo jumla ya wanafunzi watatu waliotakiwa kuhitimu na wanzao walikatisha masomo yao kwa kupata mimba.



Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top