0






Anaandika Elia Kimani kutoka Hanan'g.....
Serikali imeombwa
kuhamasisha waalimu kusomea utaalamu wa lugha 
ili kusaidia kukabiliana na uhaba wa waalimu wenye  utaalam wa kutafasiri lugha za alama kwa
watoto wenye mahiyaji maalum wanaosoma kwenye shule mbalimbali katika vitengo
vya watoto wenye mahitaji.
Shule ya msingi
Katesh A’ ni mmoja ya shule yenye kitengo cha watoto wenye ulemavu wa aina
mbalimbali lakini inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazopelekea waalimu
waliopo kushindwa kutekeleza majukum yao ipasavyo ambapo moja ya changamoto
kubwa kwao ni uhaba wa vifaa vya kufundishia na uhaba wa waalimu wataalam wa
lugha za alama.
Hata hivyo moja ya
mahitaji kwa watoto wa aina hii ni pamoja na ukaribu wa jamii kama  wanavyobainisha mbele ya umoja ya waalimu
wakuu akinamama wa shule za sekondari wilaya ya hanang ambao wametembelea shule
hii na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye dhamani kwaajili ya watoto hawa.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top