Kunguru mmoja amelazimu ndege
iliokuwa imewabeba wanajeshi wa Amisom kutoka Burundi kutua kwa ghafla
katika uwanja wa ndege wa Bujumbura nchini Burundi.Ndege hiyo ilisalia hewani kwa takriban saa moja kabla ya kutua.
Wanajeshi wa Burundi ni miongoni mwa wananjeshi wa Umoja wa Afrika wanaokabiliana na wapiganaji wa Al-Shabab nchini Somalia.
Afisa mkuu wa uwanja wa ndege wa Burundi Emmanuel Habimana amethibitisha kuwa ndege hiyo iligonga kunguru huyo mepama alfajiri.
Hatahivyo kulingana na afisa huyo hakukuwepo na tatizo lolote la kiufundi na ndege hiyo iliondoka tena.
Post a Comment
karibu kwa maoni