Mbunge
Viti Maalum Jimbo la Morogoro (Chadema), Devotha Minja ameihoji
serikali juu ya utekelezwaji wa sera ya huduma ya matibabu bure kwa
wazee.
Minja
ameyahoji hayo katika kipindi cha maswali na majibu kwenye kikao cha
sita cha Bunge la kumi linaloendelea mjini Dodoma, ambapo amesema wazee
katika kambi ya Fungafunga iliyoko mjini Morogoro wanakosa dawa na
kulazimika kununua dawa muhimu kwenye maduka ya dawa ya nje, kutokana na
uhaba wa dawa uliopo kwenye Hospitali ya mkoa wa Morogoro.
“Kambi
ya Fungafunga iliyoko mjini Morogoro inayohudumia wazee wengi hivi sasa
wanakosa huduma ya matibabu kutokana na hospitali ya mkoa wa Morogoro
kukosa dawa za kutosha, wazee wanapewa panado na dawa nyingine
wanaambiwa wakanunue kwenye famasi za nje, nataka kujua sera hii ya
matibabu bure kwa wazee inatekelezeka?,” amehoji.
Akijibu
swali la Minja, Naibu Waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile amesema serikali inatekeleza sera
hiyo kikamilifu, pia kwa sasa hakuna uhaba wa dawa kwenye hospitali za
umma, kutokana na kuongezeka kwa bajeti ya dawa kutoka bilioni 30 hadi
kufikia takribani bilioni 270.
“Serikali
kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007 imetamka wazi kwamba matibabu
kwa wazee wasiojiweza yatakuwa buree na hilo tunalitekeleza kikamilifu
lakini sambamba na hilo, hatuna uhaba wa dawa sasa hivi, bajeti ya dawa
imeongezekasana kutoka bilioni 30 hadi kufikia takribani bilioni 270
dawa zote muhimu zinapatikana, kama kuna suala mahsusi kuhusiana na
kambi hii, devotha minja ningependa kupata maelezo ya ziada ili
tushughulikie tatizo hilo,” amesema.
Aidha,
Dkt. Ndugulile amesema kwa sasa serikali iko kwenye mapitio mapya ya
sera, baada ya sera yam waka 2003 kupitwa na wakati, ili ihuishe
mahitaji ya wazee ya sasa kwa ajili ya kutunga sheria mpya.
Post a Comment
karibu kwa maoni