0
Takwimu zinaonesha kuwa Watanzania 225 huambukizwa Virusi vya Ukimwi kwa siku.

Hali hiyo inamaanisha kwamba kwa mwezi watu 6,750 huambukizwa VVU na kwa mwaka ni 81,000.

Takwimu
hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi
(TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, jana  Jumanne Machi 6, wakati akifungua
mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu uandaaji wa programu bora za
Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi.

Alisema hali hiyo ni mbaya zaidi kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.

“Asilimia 40 ya maambukizo mapya hutokea kwa vijana wenye umri Kati ya miaka 15 hadi 24 na kati yao wengi ni wanawake.

“Hii
inamaanisha kwamba katika hiyo asilimia 40 ya vijana waliopata
maambukizi mapya, asilimia 80 ni wanawake,” alisema Dk. Maboko.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top