
Hayo yameelezwa jana mjini Dodoma na
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi wakati alipowasilisha
Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria na taasisi zake
kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.
Kamati hiyo ilikuwa nchini ya
Uenyekiti wa Najma Murtaza Giga.
Profesa Kabudi ameieleza kamati hiyo
kwamba, kifungu cha 219 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Sura
ya 20, kinampatia Waziri mwenye dhamana ya masuala ya sheria mamlaka ya
kuwaachia huru wagonjwa wa akili waliotenda makosa mbalimbali ya jinai yakiwamo
ya mauaji.
Aliongeza kuwa kwa muda mrefu
wagonjwa hao walikuwa wakihifadhiwa kwenye Taasisi ya Isanga kusubiri amri ya
Waziri.
Pamoja na kuelezea hilo, Profesa
Kabudi pia alianisha mafanikio mbalimbali yaliyotekelezwa na wizara pamoja na
taasisi zake katika suala zima la utoaji na usimamiaji wa haki katika kipindi
cha bajeti cha 2017/2018.
Baadhi ya mafanikio hayo ni kwa
Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika uendeshaji wa
mashauri ya daawa ilipata ushindi katika mashauri 82 yaliyokuwa na thamani ya
Sh 1,064,581,955,743.
Kwa mujibu wake, ushindi huo
umewezesha pamoja na mambo mengine maamuzi ya serikali pamoja na sheria za nchi
kutobadilishwa kwa msingi wa kukiuka Katiba.
Mafanikio mengine aliyoyataja ni
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea na utoaji wa ushauri wa
kisheria kwenye mikataba na makubaliano mbalimbali yanayofanywa na Wizara Idara
na Taasisi za Serikali.
Katika eneo hilo, hadi kufikia
Februari mwaka huu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilifanya uhakiki na kutoa ushauri
wa mikataba 691 yenye thamani ya Sh 1,720,026,713,823 na Dola za Marekani
1,0884,472,366, mikataba hiyo ilihusu ununuzi, ukarabati wa majengo, utoaji wa
huduma za jamii na ujenzi wa barabara.
Aidha, kwa upande wa mali
zilizotaifishwa ni pamoja na kilogramu 24.5 za dhahabu yenye thamani ya Sh
2,012,357,164 na fedha za kigeni kutoka mataifa 15 zenye thamani ya Sh
908,019,979.
Mali nyingine zilizotaifishwa ni
pamoja na magari matano ya kifahari aina ya Range Rover Vogue na moja aina ya
Audi yaliyokamatwa katika bandari ya Dare s Salaam yakisafirishwa kama nguo za
mitumba.
Post a Comment
karibu kwa maoni