Mkurugenzi
Mtendaji wa MSD Laurian Bwanakunu amesema baada ya kuongezewa bajeti
yao kufikia bilioni 250 kwa sasa MSD wanasambaza dawa zenye thamani ya
bilioni 18 na lengo ni kufikia bilioni 21 ikifika mwezi Julai.
Bwanakunu
ameyasema hayo leo Jumatatu, Machi 26 katika hafla uzinduzi wa magari
mapya 181 ya MSD kwa ajili ya kusambaza dawa na vifaa tiba.
Aidha
amefafanua kwamba licha ya usambazaji huo wa dawa bado changamoto
imekuwa katika makadirio ambapo kituo cha afya kinaweza kusema
"wanahitaji makopo 20 ya panadol wakati mahitaji ni makopo 60, dawa
zikiisha tunalaumiwa MSD."
Pamoja
na hayo Mkurugenzi wake amepongeza na kushukuru kwa magari yaliyotolewa
ambapo amkiri kwamba ni kiwango kikubwa kuwahi kupokelewa tangu
kuanzishwa kwa MSD.
"Tangu
MSD ianzishwe mwaka 1994 hatujawahi kupokea magari mengi kiasi hiki,
gharama yake ni bilioni 20.7. Sasa tutakuwa na jumla ya magari ya
kusambaza dawa na vifaa tiba 213, hii ni hatua kubwa sana katika kutanua
wigo na uharaka wa kazi zetu," amesema Bwanakunu.
Post a Comment
karibu kwa maoni