0
Image result for PAPA FRANCISKatika mahojiano na gazeti la kila siku la La Repubblica, kiongozi wa kanisa katoliki papa Francis amenukuliwa akisema hakuna jahanam ambako roho za wenye dhambi zitaadhibiwa milele.

Francis alisema kwamba baada ya kifo , roho za watu ambao wanatubu zitapata msamaha kutoka kwa Mungu na kujiunga na zingatio la tafakari ya Mwenyezi Mungu, lakini wale ambao hawatatubu, na kwa hiyo hawatapata msamaha, watatoweka.

Ameongeza kwamba moto hakuna, kile kilichopo ni kutoweka kwa roho zenye dhambi. Papa alihojiwa na mwandishi habari maarufu nchini Italia kabla ya sikukuu ya pasaka kuhusu imani na dini.
Papa Francis pia alitarajiwa kufanya kanuni ya kidini ya kuosha miguu inayofanyika kabla ya sikukuu ya pasaka katika jela ya Regina Coeli mjini Rome leo huku kukiwa na ulinzi mkali katika mji huo mkuu wa Italia.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top