Kadinali Pengo ameyasema hayo wakati akiadhimisha ibada ya Jumapili ya matawi huko Bagamoyo katika tamasha la vijana.
"Katika
wiki chache zilizopita watu wamekuja kwangu wakaniuliza unaionaje ile
barua ya Maaskofu kuhusu Kwaresma mwaka huu? Ninazungumzia hilo na wala
mtu asiende aka-quote kitu kingine ndio maana nataka kusema wazi
kabisa:-
"Barua
ile ijapokuwa hata jina langu mnaliona limeandikwa pale kwamba na mimi
ni mmoja wa waandishi au watamkaji...mimi nimeipokea, baadhi yenu
mmeshaipokea.
"
Kwahiyo sioni namna gani mimi naweza kuwa mwandishi au mhubiri kwenu wa
ile barua ambayo imetungwa labda na maaskofu...naamini na baadhi ya
maaskofu lakini mimi mwenyewe hata nilikuwa sijaiona, hata nilikuwa
sijaambiwa kuna kitu cha namna hiyo kinakuja.
"Tuelewane
vizuri, ninaposema hivi sitaki kusema ile barua ni mbaya. Moja tu ni
kwamba barua nzima imechanganya vitu viwili; Mwalimu angekuwepo angepiga
kelele Maaskofu msichanganye Dini na Siasa.
"Angepiga
kelele sana kuhusu waraka huu katika nyakati zake. Na hilo nawambia
sina hofu, muende mkamwambie mtu yeyote nimesema hivi. Ndio wala msione
aibu, najua labda hata wengine mmekunja nyuso, kunjeni tu lakini huo
ndio msimamo wangu.
"Zipo
sehemu katika waraka huo zinazochanganya Dini na Siasa na si kazi ya
maaskofu ni kazi yenu wanasiasa mkiwa ni wa CHADEMA, mkiwa ni wa CCM
lakini haiwezi kuwa kazi yangu mimi.
"Siwezi
kwanza nikaanza kuchambua na ku-criticize Serikali katika mambo yaliyo
yake; sikupewa mamlaka hayo. Na kwanini niwe padri mpaka nikubali kuwa
Askofu na huku kumbe wito wangu ni siasa?
"Itakuwa
namsaliti hata yule aliyenipa wito huu. Tuchambue yale yanayohusu imani
yetu katika ule waraka. Yale ambayo moja kwa moja yanahusu imani yetu
Katoliki na tuyashike tuyazingatie kwa dhati kabisa.
"Lakini
yale ya kuanza kusema Serikali ya awamu ya 5 inagandamiza uhuru
inafanya nini...wewe Askofu uhuru wa kisiasa umeujua wapi? Umeujuaje? Na
mambo ya ndani ya kisiasa huyajui na bado uje kutamka...nadhani
tumeelewana.
"Yapo
yaliyo mema mazuri kabisa katika waraka ule ingawaje sikujuia kama
yameandikwa lakini siwezi kukataa yaliyo mema kwa sababu sikujua.
"Yanaendelea kuwa mema mpaka kesho na keshokutwa. Lakini yale ambayo yanachanganya Dini na Siasa hayo siwezi kuyakubali.
"Nyerere
alifanya indoctrination kubwa mno kwa watu wa umri wetu. Mtu huwezi
ukathubutu na ukalala salama usiku. Watu wa umri wangu ukichanganya dini
na siasa utaota vitu vya ajabu utakosa usingizi(vicheko)
"Sasa
ninyi vijana ninalotaka ni hili kwamba na ninyi mkichanganya dini na
siasa muote vitu vibaya kama hivyo..muote vitu vibaya kabisa hata muone
mnachungulia kaburi katika ndoto.
"Sisi
sio wanasiasa tunahitaji wanasisia mtuendelee wale tunaokuwa wito huo.
Wale tunaotaka kuwa mama wakuu, mababa padri, maaskofu. Fuateni wito
kulingana na misimamo yake ya kiimani."
Post a Comment
karibu kwa maoni