0
https://youtu.be/kSKZsexPfZ0
Baada ya vuta nikuvute ya ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa katika mkoa wa Manyara,hatimaye bingwa wa Mkoa amejulikana ni Usalama Sports Club.
Akimtangaza bingwa wa mkoa katika ligi daraja la tatu iliyomalizika mwanzoni mwa wiki hii katibu wa Mashindano Yusuph Mdoe amesema kuwa baada ya Usalama kuandika barua na kuonekana wanacholalamikia kina mashiko wamempa ubingwa.
Usalama waliandikia barua Kamati ya Mashindano inayosimamiwa na chama cha soka mkoa MARFA kulalamika juu ya kitendo cha upangaji wa matokeo kati mechi ya Firestone ya kiteto dhidi ya Morning Star ya Mbulu mchezo uliomalizika kwa Firestone kushinda kwa idadi ya mabao mengi 8-2 Morning Star.
Mdoe ameeleza kuwa Usalama ametangazwa bingwa wa mkoa Manyara baada ya mchezo wa Morning Star na Firestone kufutwa kwa kuonekana kupangwa kwa matokeo kitendo ambacho ni kinyume na taratibu za mashindano.
Akizungumza na kipindi cha Sports Power kinachorushwa  redio Manyara Fm Mlezi wa Usalama Sports Club Mkuu wa upelelezi na Makosa ya jinai mkoa wa Manyara SSP Joshua Mwafulambo amesema kwa sasa ni mwendo wa kusonga mbele huku akiwataka wadau wa Soka kuisapoti timu kwa nguvu zote kwa kuwa ndio timu pekee ndani ya Manyara iliyopiga hatua hadi daraja la pili[Kanda].
“Malengo ya Timu hii inayomilikiwa na wananchi kwa kushirikiana  na jeshi la polisi kupitia vikundi shirikishi na polisi jamii, Mkoa wa Manyara ni kufika ligi kuu na kushuhudiwa timu mbalimbali zikifika katika mkoa wetu kucheza soka.’alisema Mwafulambo.
Hata hivyo Morning Star na Firestone zote kwa pamoja zimepigwa faini ya shilingi laki tano [500,000] na kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka mitatu.
Mrara Fc pamoja na Bm Fc zenyewe zimekumbwa na adhabu ya kufungiwa miaka mitatu baada ya kushindwa kuhudhuria  uwanjani Mrara akishindwa kwenda uwanjani mchezo miwili ,mmoja dhidi ya Bm Fc na mwingine dhidi ya Fire Stone bila kutoa taarifa yeyote na Bm Fc alishindwa kuhudhuria katika mechi dhidi Fire Stone.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top