0
Image result for kamanda sengaKamandawa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, Agustino Senga  amesema
wamejipanga vizuri katika kuimarisha hali ya usalama ndani ya mkoa wa Manyara katika sikukuu hii ya Pasaka na kudai atakayethubutu kufanya vitendo vya
kiharifu atachukuliwa hatua kali.

Kamanda Senga ameeleza hayo leo (Machi 31, 2018) wakati alipokuwa
anazungumza katika kipindi cha jungu kuu redio Manyara Fm Babati mjini  na kusema kulingana na uzoefu waliokuwa nao wamejipanga kuimarisha usalama kwa hali ya juu ili wananchi waweze kusherehekea kwa amani na utulivu.

"Jeshila Polisi litahakikisha wananchi wa Manyara wanasherehekea sikukuu hii kwa amani na utulivu na kwa kuwa uzoefu unaonesha kwamba mara nyingi katika
sherehe kama hizi watu wenye nia ovu wanajiandaa kufanya vitendo vya
kihalifu ikiwa na pamoja na kufanya ujambazi ili kujipatia vipato kwaajili ya kusherehekea sikukuu", amesema Senga.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top