0
Nembo ya FacebookMmiliki wa Facebook amewaambia maseneta wa Marekani kuwa kampuni yake imekuwa ikipambana na watumiaji wa Warusi wanaotaka kuutumia vibaya mtandao huo wa kijamii
" Haya ni makabiliano ya kijeshi. Watarekebika ,"alisema he said.
Bw Zuckerberg alikua akijibu maswali kuhusiana na sakata ya matumizi mabaya ya data za kibinafsi maarufu kama Cambridge Analytica.
Pia amefichua kuwa Robert Mueller, kutoka baraza maalum linalochunguza madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani wa Mwaka 2016 aliwahoji wafanyakazi wa Facebook.
Bwn Zuckerberg yeye hakuwa miongoni mwa watu waliohojiwa na ofisi ya Bw Mueller
Lakini aliongeza kuwa : "kazi yetu na baraza maalum ni ya siri na ninataka kuhakikisha kwamba katika kikao cha wazi sifichui chochcote juu ya taarifa za siri.
Mwezi Februari, Ofisi ya Bw Mueller ilishtakiwa na Warusi 13 kwa kudukua taarifa za uchaguzi wa mwaka 2016, pamoja na makampuni matatu ya Urusi.
Bw Zuckerberg amesema kuwa kampuni yake sasa imetengeneza nyenzo za kubaini akaunti gushi.
Awali Mtendaji mkuu wa mtandao wa kijamii Facebook, Mark Zuckerberg ameomba msamaha kwa kamati ya Seneti ya Marekani kwa kuruhusu makampuni kadhaa kutumia vibaya data binafsi za jukwaa hilo kisiasa.
Mark Zuckerberg alijitetea kwa muda wa saa tano katika jopo la wasikilizaji kutoka bunge la seneti la Marekani linalohusika na masuala ya biashara na kamati ya mahakama.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top