0
Artwork: Tiangong-1Shirika la Anga la Ulaya, ESA, limesogeza nyuma muda ambao chombo cha anga za juu cha China kinatarajiwa kuingia katika anga la dunia, ambao ni kati ya Jumapili jioni na Jumatatu asubuhi. Chombo hicho, Tiangong-1, kilipelekwa angani mwaka 2011, na hakiwezi kurejeshwa duniani chini ya uangalizi wa wanasayansi kwa sababu kiliharibika miaka miwili iliyopita. Awali chombo hicho kilitarajiwa kuingia duniani Jumapili jioni, lakini hali ya anga ilibadilika ghafla na kupunguza kasi yake. Wanasayansi wanatabiri kuwa Tiangong itaungua moto punde tu ikiingia katika anga la dunia, lakini baadhi ya vipande vyake vitaanguka duniani, vikitapakaa katika eneo la kilomita nyingi za mraba. Wataalamu hao wanabashiri kuwa kuna uwezekano mkubwa kwamba vipande vivyo vitaanguka baharini. Chombo hicho kina uzito wa tani 8.5.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top