0
Baada ya kushuhudia vilabu vikubwa kama vya Simba na Azam FC vikiaga michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup, leo ilikuwa ni zamu ya Dar es Salaam Young Africans kucheza mchezo wao wa robo fainali ya michuano hiyo dhidi ya Singida United.
Yanga walilazimika kusafiri hadi Singida kucheza mchezo wao wa robo fainali dhidi Singida United katika uwanja wa Namfua, hiyo ni baada ya droo kuonesha Yanga anapaswa kucheza ugenini, mchezo huo dakika 90 zilimalizika kwa sare ya 1-1, goli la Yanga likifungwa na Yusuph Mhilu dakika ya 23 na Singida likafungwa na Kenny Kelly dakika ya 83.
Hivyo baada ya sare ya 1-1 game ikalazimika kuamuliwa kwa mikwaju ya penati ndio, Singida wakapata ushindi wa penati 4-2, Emmanuel Martin na Papy Tshishimbi ndio waliokosa penati kwa upande wa Yanga, kwa matokeo hayo Singida atacheza nusu fainali dhidi ya JKT Tanzania.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top