0



Wanaume nchini wametakiwa kushiriki kikamilifu kusimamia afya ya mama na mtoto ili kuepuka vifo vinavyotokana matatizo ya uzazi na utapiamlo.
Hayo yameelezwa na mtaalamu wa afya na lishe kutoka shirika la World Vision Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara Joan Msuya wakati wa wakihitimisha mafunzo ya wiki tatu kwa watoa huduma za afya ngazi ya jamii Tarafa ya Gorowa wilayani hapa.
Mtaalamu huyo amesema matarajio ya shirika hilo kupitia mafunzo waliyoyatoa,wanaamini jamii itahamasishwa pamoja na kutoa elimu sahihi za afya na Lishe katika ngazi ya kaya na katika vituo vya kutolea huduma.
Joan ameeleza kuwa wanategemea ushiriki mkubwa kwa wanaume katika masuala ya afya na Lishe ya mama na mtoto na hatimaye kupunguza vifo vya watoto pamoja na wanawake vitokanavyo na uzazi na matatizo ya utapiamlo kwa watoto tarafa ya Gorowa.
Akizungumza baada ya kuwatunuku vyeti walipata mafunzo hayo,mkurugezi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Babati Hamis Idd Malinga amewataka walipata mafunzo hayo wakawe chachu ya kuibadilisha jamii na kupunguza matatizo ya Uzazi na utapiamlo kwa watoto.
Shririka la Worl Vision Tanzania [WVT] limekuwa likiendesha program mbalimbali za maendeleo ya jamii katika maeneo tofauti tofauti kupitia miradi yake 45 iliyopo Tanzania.
Miongoni mwa maeneo ya mradi ni pamoja na Gorowa ADP ambayo ipo ndani ya Halmashauri ya Babati mkoani Manyara  na imekuwa ikiwawanufaisha wanajamii wa Gorowa  kwa kuwasaidia kujikwamua kiuchumi katika kuwapatia wana vikundi mikopo,kujenga shule kupitia mradi wa watoto tusome,kutengeneza kambi za watoto za kujifunzia,kununua vitabu na kuvisambaza mashuleni na kuwawezesha watoto wanaoishi katika mazingira magumu katika mahitaji muhimu ya watoto ikiwa ni pamoja na elimu.
Aidha shirika hilo kwa kujali umuhimu wa Mazingira limewahimiza wakazi wa kata ya Riroda kutunza misitu kwa  kuwapatia miche ya miti 35,000 ili kuboresha hali ya hewa.
Shirika llimejenga mifereji ya kumwagilia katika vijiji vya Sangara na Ayasanda iliyogaharimu ziadi ya Tshs.152,000,000.
Kwa upande mwingine shirika limejenga chuo cha mafunzo ya Ufundi [VETA] katika kijiji cha Ayasanda ambapo hivi karibuni kitakabidhiwa kwa serikali ili kuwezesha vijana kupata mafunzo mbalimbali ya Ufundi na hatimaye waweze kujiajiri wenyewe.
Vile vile shirika liko mstari wa mbele katika kuboresha Afya na lishe  ya Jamii hususani kwa Mama na mtoto,na Katika kuhakikisha afya na lishe ya Mama na Mtoto inaborshwa shirika limeendelea kutoa mafunzo jumuishi ya afya na lishe kwa watoa huduma za afya katika ngazi za jamii na vituo vyote vya afya katika kata ya Gorowa .
‘Lengo la kuwapatia mafunzo WAJA ni  ili wapate ujuzi na elimu ya lishe kuweza kuleta mabadiliko chanya ya afya na lishe katika jamii’.alisema Joan
Katika mafunzo hayo jumla ya WAJA thelethini na tano [35] pamoja na wasimamizi wao saba [7] kwenye vituo vya kutolea huduma na wasimamizi wawili kutoka CHTMT wamepata mafunzo hayo.
Washiriki hao wakizungumzia mafunzo hayo waliyopatiwa na wawezeshaji kutoka wizara ya afya,ustawi wa jamii,jinsia wazee na watoto wamesema kuwa yatawawezesha kuisaidia jamii iliyokuwa haina uelewa wa lishe kwa Mama na mtoto.
‘Jamii zetu hazijui ni muda gani motto anapaswa kunyonyeshwa baada ya kuzaliwa,hivyo kwa mafunzo haya tuliyoyapata tutayapeleka kwa kina mama ili wawanyoshe watoto wao kwa muda wa siku 1000’. Walisema WAJA.
Baada ya mafunzo hayo walipatiwa mizani saba za kisasa zenye thamani ya shilingi milioni 10,380,000 zenye uwezo wa kupima uzito wa Mama na motto kwa wakati mmoja hatua inayorahisisha utendaji wa kazi katika vituo vya afya.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top