0

Image result for MAJI SAFI 
Wanakijiji 2,510 wa kijiji cha Sangara kata ya Riroda wilaya ya Babati Mkoani Manyara wanatarajia kuondokana na tatizo la maji pindi mradi wa maji wa shilingi milioni 290,630,517 utakapokamilika.
Mkuu wa wilaya ya Babati Raymond Mushi akizungumza katika majadiliano ya mradi huo wa maji na usafi wa Mazingira katika kijiji cha Sangara amewataka wakazi wa kijiji hicho kutunza mradi huo kwa uhai wa Binadamu na viumbe hai na wadau waliofanikisha kila mmoja atimize wajibu wake ili mradi uendelee kuwepo.
Mradi huo unaosimamiwa na wadau watano ikiwemo Halmashauri ya wilaya ya Babati UTT-MFI,WATER AID TANZANIA,eWATER PAY LIMITED na HABITAT FOR HUMANITY TANZANIA unatarajia kukamilika mwezi March 2019 kama anavyoeleza mkurugenzi wa  WATER AID TANZANIA Dr. Ibrahim Kabole 'Tayari tumeshafanya utafiti na kubaini vyanzo vya maji lakini niwaombe wakaazi wa Sangara kutunza vyanzo vilivyopo ili kuepuka tatizo la maji'.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Martin Duuma Masong’ anaeleza kuwa kwa sasa wanafuata maji umbali mrefu hivyo kushindwa kufanya shughuli za maendeleo.
Image result for water aidImage result for water aid

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top