0
Mamlaka ya  Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Babati  (BAWASA) limemkamata  mteja wao mwenye mita yenye jina Fatuma Mpore baada ya kugundulika kuwa  wanaliibia Maji shirika hilo.

Akizungumza wakati wa operesheni hiyo iliyohusisha pia jeshi la polisi katika Mtaa wa Mruki mjini Babati Meneja wa Ufundi Bawasa Eng.Sebastian Honlathi  amesema walipata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa kuna mtu kajiunganishia maji kinyemela ndipo walipofika katika eneo la tukio na kukuta laini iliyokuwa inaelekea nyumba ya jirani ikiwa imefunguliwa na kuunganishwa mpira uliokuwa ukipandisha maji katika nyumba hiyo inayotengeneza pombe za kienyeji.

Hata hivyo walimkuta kijana mmoja akiendelea kutumia maji hayo kuosha mtama huku yakiendelea kumwagika chini kwa wingi,na baadaye alivyogundua ni wahusika wa Bawasa alikimbia.

Hata hivyo inafahamika kuwa nyumba iliyokutwa inafanya wizi huo ni ya Diwani wa viti Maalumu Babati mjini Fatuma Mpore na katika nyumba hiyo anaishi mdogo wake.
Eng Sebastian amesema matukio ya watu kuiba maji tangu mwaka juzi mpaka sasa yamefika ishirini na mbili na kuongeza kuwa wanawachukulia hatua mbalimbali za sheria ikiwemo kuwapiga faini ambayo ni kuanzia shilingi laki tano hadi milioni kumi kulingana na ukubwa wa kosa.

Mkurugenzi wa Bawasa Iddy Yazidi Msuya alisema“Tena watu kama hawa ndio wa kwanza kulalammika bili kubwa na mambo mengine,sheria ichukue mkondo wake jamani tumechoka.”Alisema Msuya.
“Bawasa tunajiendesha kwa kuzalisha Maji na kuhudumia wananchi na gharama zote hizo ni kutokana na mapato yanayopatikana ndani ya shirika kutokana na Ankara ya Maji inayolipwa na mteja.

“kwahiyo inapotokea watu wanafanya hujuma za aina yoyote ieleweke kwamba shirika linaingia hasara kubwa ambayo haiwezi kuvumiliwa kwa namna yoyote.” Alisema Bwana Sebastian.

Ameeleza kuwa wizi huo  wameugundua baada ya kupata taarifa toka kwa wasamalia wema juu ya kuwepo kwa maunganishio yaliyofanywa mapema asubuhi ya leo mei 25.2018 na kwamba sio mara ya kwanza nyumba hiyo kujiunganishia maji Kinyemela ambayo yanatumika  katika kutengeneza Pombe za asili.

Alipoulizwa kama wanautaratibu wa kulipa Ankara zao kila mwezi kwa Maji ya BAWASA wanayotumia, alisema bili inakujaga  kuanzia shilingia 1700 na kuendelea   na analizipa.


Akijitetea mbele ya watu wa Bawasa mama huyo ambaye jina lake halikupatikana mara moja alisema ni mara siku mbili tu ndio alizojiunganishia maji huku Mafundi wa Bawasa wakitambua kuwa sio mara ya pili au ya tatu nyumba hiyo kujiunganishia maji kwa njia zisizo halali huku ya kwao wakiwa hwayatumii kuzuia bili ya maji kuwa kubwa.

Kesi hiyo imefunguliwa katika kituo cha polisi cha kati  Babati mjini  na shauri litapelekwa Mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa na kutolewa hukumu.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top