0
Image result for KAMOGA 
Timu ya soka ya Dongobesh fc imetwaa ubingwa wa kombe la kurugenzi baada ya kuifunga timu ya Rema 1,000 fc mabao 3-1 kwenye mchezo wa fainali uliyopigwa katika uwanja wa shule ya msingi Haydom wilayani Mbulu mkoani hapa.
Katika mchezo huo mabao ya Dongobesh fc yalifungwa na wachezaji Antipas Vincent dakika ya 35,Toroti Thobias dakika ya 70 na Idd Twalib dakika ya 80 wakati bao la kufutia machozi ya Rema 1,000 lilifungwa na Lawrence Marco dakika ya 55.
Mgeni rasmi katika mchezo huo wa fainali alikuwa katibu mkuu wa wizara ya habari utamaduni,sanaa na michezo Suzan Mlawi aliwataka vijana kujishughulisha na michezo hili kupata vijana ambao wataitangaza vyema taifa kwenye michezo.
"Mtumie fursa ya kuwepo kwa Michezo kwenye maeneo yenu mnayoishi ili muweze kupiga hatua kwa kushiriki ipasavyo na kujindeleza kwa bidii" alisema Mlawi.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu ambaye ndie mwandaaji wa mashindano hayo Hudson Kamoga alisema michuano ilishirikisha jumla ya timu 10 na lengo ilikuwa ni kusisitiza uzalendo kwa vijana na jamii kupenda nchi yao pamoja na kuibua vipaji.
"Kwa muda huu wa wiki moja Haydom imesisimka kwa kupata burudani,mafunzo ya ujasiriamali na kusitizwa uzalendo kupitia kauli mbiu Niwakati wa kuwa mzalendo wa kujenga nchi yetu, Uvivu ni sumu ya maendeleo" alisema Kamoga.
 Alisema mishoni mwa mwaka huu watafanya tena mashindano hayo kwenye kata ya Haydom ambayo ndio makao makuu mapya halmashauri ya wilaya hiyo.
Kwa upande wa zawadi mshindi wa kwanza Dongobesh fc walipata kombe jezi seti moja na mipira miwili,mshindi wa pili Rema 1,000 fc walipata jezi seti moja na mpira mmoja huku mshindi wa tatu Young boys wenyewe wakapata jezi seti moja.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top