0
Magavana wa nchi za Afrika wametakiwa kuwa na utayari wa kuzisaidia nchi zao kutatua changamoto za kiuchumi na kuhamasisha maendeleo endelevu ili kuendana na mapinduzi makubwa yanayotokea kote Duniani kwa kuhamasisha ukuaji wa viwanda.
Rai hiyo imetolewa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika- AfDB, Dkt. Akinumwi Adesina, wakati wa Mkutano wa 6 wa jukwaa la ushirikiano kati ya Jamhuri ya Korea Kusini na Nchi za Afrika uliolenga kujadili namna bora ya kuchochea ukuaji wa sekta ya viwanda katika Nchi za Afrika.
Wadau wa Mkutano huo uliofunguliwa na Makamu wa Waziri Mkuu wa Korea Kusini  Bw. Kim Dog – Yeon, wamezitaka nchi za Afrika  kuhakikisha zinafanya mapinduzi  ya kiuchumi kwa  kuwekeza kwenye viwanda na miundombinu kwa kuwa  itasaidia uchumi wa nchi kukua kwa kasi na  kuleta maendeleo yenye tija.
Vilevile nchi za Afrika zinahitaji kuwa na na ushirikiano wenye manufaa na wahisani ikiwemo nchi ya  Jamuhuri ya Korea Kusini  ili kuharakisha maendeleo hayo ya kiuchumi kwa kubadilishana uzoefu na kubaini fursa za ukuaji wa uchumi utakaochochea ushirikiano huo.
Afrika inafursa nyingi za kukuza uchumi kwa kuwa inarasilimali za kutosha kwa takribani sekta zote muhimu za maendeleo ikiwemo ya madini, kilimo, mifugo na Uvuvi.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top