0
Mkurugenzi Mkuu wa NYS Richard Ndubai akiwa mahakamani JumanneWatuhumiwa 24 walioshtakiwa kuhusiana na kashfa ya ufujaji wa pesa katika Shirika la Vijana wa huduma kwa Taifa (NYS) watakaa rumande kwa wiki moja.
Jaji ameamuru wazuiliwe hadi wiki ijayo ambapo uamuzi wa kuachiliwa kwa dahamana utatolewa.
Miongoni mwa walioshtakiwa jana ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Vijana na Jinsia Lilian Mbogo Omollo na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Richard Ndubai.
Walikamatwa na wengine wakajisalimisha kwa polisi Jumatatu wiki hii na kisha kufikishwa kortini Milimani, Nairobi jana.

Jumuiya ya Kimataifa yapongeza hatua za kisheria Kenya

Wajumbe kutoka mataifa ya kigeni wameisifu serikali ya nchi hiyo kwa msako unaoendelea dhidi ya ufisadi.
Kwenye taarifa ya pamoja, wajumbe hao wakiwemo wa Marekani na Uingereza, wamesema kwamba watakaopatikana na hatia wachukuliwe hatua, ikiwemo kunasa mali yao iliyotokana na ufisadi.
Wajumbe hao wanaowakilisha mataifa kumi na saba walisema kwamba kwa muda mrefu ufisadi umedhoofisha demokrasia nchini Kenya, na kwamba huu ulikuwa wizi mkubwa.
Walipongeza kufikishwa mahakamani kwa watu 24 kwa mashtaka ya kuhusika na ufujaji wa ndola milioni 80, na kutaka kesi ifanyike kwa haraka tena kwa haki.
Upande wa mashtaka ulipinga washukiwa kupewa dhamana kwa misingi ifuatayo:
  • Lilian Omollo: Alikuwa katibu mkuu katika wizara ya utumishi kwa umma na masuala ya vijana na ya kijinsia na ndiye aliyekuwa ni afisa mhasibu wakati malipo hayo ya ulaghai yalipotolewa
  • Sammy Mbugua Mwangi: Mkuu wa hesabu katika wizara ya utumishi wa umma. Alikuwa mtu wa mwisho kuidhinisha malipo ya ulaghai kwa mabenki kupitia intaneti na alizilipia vocha kadhaa zisizokuwa na saini stahiki kama ilivyoshuhudiwa katika vocha zilizopatikana.
  • Micheal Ojiambo: Ni mkurugenzi wa usimamizi katika wizara na ndiye aliyewasilisha kwa katibu mkuu katika wizara, vocha za malipo ambazo hazikuwepo kwenye orodha ya uthibitisho wa kamati na kuziidhinisha kuwa sawa kama ilivyoshuhudiwa katika ilani za kuwasilisha vocha hizo.
  • Clement Murage: Alikuwa mhasibu mkuu wa zamani aliyekuwa na jukumuu kuu katika utoaji wa malipo hayo ya ulaghai aliyesaini kuidhinisha malipo kwa vocha na alikuwa mmojawapo ya wanakamati ya pili ya uthibitisho na hakuthibitisha uhalisi wa malipo hayo ya ulaghai ya vocha.
  • Richard Ethan Ndubai:Ni mkurugenzi mkuu wa shirika la NYS na ndiye aliyesaini kuidhinisha malipo hayo ya ulaghai.
Upande wa mashtaka ulikuwa umepinga kuachiliwa kwao ukisema wanaweza kutoroka au kukosa kurejea mahakamani wakati wa kusikizwa kwa kesi dhidi yao.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top