0
Uongozi wa Yanga umetangaza rasmi tarehe mpya ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa klabu hiyo ambayo ni Juni 10 2018.

Awali uongozi ulitangaza mkutano kufanyika Juni 17 2018, tarehe ambayo inaweza ikawa siku kuu ya Idd baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kumalizika.

Kuelekea mkutano huo, wanachama wote wamearifiwa kwenda na kadi za zamani pamoja na za sasa zikiwa hai, kwa maana ya kwamba ziwe zimelipiwa ada.

Inaelezwa kuwa moja ya ajenda zitakazojadiliwa kwenye mkutano huo ni pamoja na suala la mabadiliko ya klabu kutoka mfumo wa zamani wa kuendeshwa na wanachama kwenda kwenye uwekezaji.

Tayari maandalizi ya mkutano huo yameanza ambapo juzi wajumbe wa Kamati ya Utendaji Yanga walikutana kwa ajili ya kujadili mchakato mzima utakavyoenda.

Post a Comment

karibu kwa maoni

 
Top